×

Mshtuko mali za Mbowe Kupigwa Mnada

TANGAZO la kupigwa mnada kwa mali za Kampuni ya Mbowe Limited inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, limeibua mshtuko wa aina yake.

 

Mali hizo zinatarajiwa kupigwa mnada baada ya kushikiliwa kwa miaka mitatu. Mali hizo ni zile zilizokuwa kwenye Ukumbi wa Disco wa Bilicanas ambao mwaka 2016 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilichukua kwa madai ya kutolipwa kodi kwa miaka 20.

Hadi vifaa hivyo vinazuiliwa kodi iliyokuwa inadaiwa ilikuwa shilingi bilioni 1.1. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joshua Mwaituka alithibitisha uwepo wa mnada huo na kueleza kuwa utafanyika kesho.

Alivitaja baadhi ya vitu vitakavyopigwa mnada kuwa ni viti, meza, makochi, makabati, taa, majukwaa na vifaa vingine vilivyokuwa ndani ya ukumbi huo. Alisema mnada huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye ghala la NHC, karibu na geti namba 3 la Bandari ya Dar es Salaam.

 

Waziri Kanyasu Azungumzia Safari ya Kitalii ya MAGAMBA