×

Kwa Shamsa Hakuna Kuangalia Nyuma

Move on! Mwigizaji mahiri Wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford Amefunguka kuwa, mwanamke akishaachana na mwanaume, hakuna sababu ya kurudi nyuma wala kukumbuka chochote cha kwake.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Shamsa alisema mara nyingi wanawake wanapotoka kwenye uhusiano wanaona ni kazi ngumu kupita kwenye kipindi hicho, kumbe wanatakiwa wakitoka ndiyo iwe imeisha hiyo.

 

“Kama Umechana na mtu hakuna sababu ya kujadiliana na wenzako mambo yake, wewe songa mbele,” alisema Shamsa.

Stori: Imelda Mtema, Dar