
JARIDA maarufu la Forbes limeripoti kuwa staa wa muziki kutoka Marekani, Taylor Swift, ndiye mwanamuziki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani miongoni mwa walio chini ya umri wa miaka 30 .

Jarida hilo limesema jana (Jumatano) kwamba anaingiza Dola milioni 185 kwa mwaka (Sh. bilioni 425) , akifuatiwa na mwanamitindo Kylie Jenner anayeingiza kiasi cha Dola 170 (Sh. bilioni 390) huku rapa Kanye West akishika namba tatu kwa kuingiza kiasi cha $150 (Sh. bilioni 343).
Mhariri wa Forbes, Zack O’Malley Greenburg amesema kuwa sehemu ya mapato ya Taylor Swift imetokana na maonyesho ya jukwaani.
