×

SOULJA BOY APUNGUZA MARAFIKI BAADA YA KUTOKA JELA

Related image

STAA wa rap wa Marekani,  Soulja Boy,  sasa amekuwa mtu mzuri baada ya kutoka jela akiwa ametumikia kifungo cha miezi mitatu kati ya kifungo cha miezi minane

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Soulja Boy ameamua kuishi kitofauti baada ya kutoka jela ambapo amepunguza marafiki na amepunguza muda wa kutumia mitandao ya kijamii.

Hadi sasa, katika  mitandao yake ya kijamii ya Twitter na Instagram, hajaweka chochote tangu alipoachiwa Julai 14 mwaka huu,

Hata hivyo, staa huyo ataendelea na adhabu yake kwa kufanya kazi za kijamii kwa siku 265.