
KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuwa hana wasiwasi wowote na mastraika wake kwani wanampa raha.
Akili yake yote sasa ameielekeza kwenye ukuta. simba ambayo ipo kambini nchini Afrika Kusini zilizpo timu kibao za Afrika, jana iliwapiga Platinum stars mabao 4-1. Jumamosi simba itavaa wapinzani wa Yanga, Township Rollers mjini hapa.
Juzi simba ilicheza dhidi ya Orbret TVET na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 na jana ilicheza dhidi ya Platinums stars. Kocha huyo alifunguka kuwa kwa sasa ana muda mfupi wa kutengeneza timu hivyo lazima awe makini na kuangalia viwango na sio matokeo.
“Kwenye mechi hizo mimi siangalii matokeo ninachoangalia ni jinsi gani wachezaji wangu wanajituma na kutengeneza muunganiko mzuri kama mechi ya TVET niliangalia zaidi eneo la ulinzi kuona kama tupo imara.

“Kwa mechi hizo nina dili zaidi na kujenga timu na sio matokeo kutokana na majukumu ambayo yapo mbele yetu wala siangalii matokeo wala nini,” alisema Mbelgiji huyo. simba itaanza kampeni yake kimataifa, Agosti 9, mwaka huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.