×

Breaking News: Lugola Amuondoa Madarakani RTO Arusha

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amemuondoa madarakani mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa madai ya kupuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa.

 

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Julai 28, 2019 na ofisi ya mawasiliano ya wizara hiyo imeeleza kuwa licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo, Lugola amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake, kumchukulia hatua za kinidhamu RTO huyo ili iwe fundisho kwa trafiki.

 

Lugola amesema amemshuhudia Bukombe katika video inayosambaa mitandaoni alipokuwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na hakuyatekeleza.

 

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Malinyi mkoani Morogoro leo Lugola amesema hatoi maagizo ya kisiasa, hutuo yanayomsaidia Rais John Magufuli katika kazi zake.

ONA HOTEL ALIYOLALA MAGUFULI YA DOLA 3000 RUFIJI..!