Amberr Washington Aifagilia Global Group (Picha +Video)
Global Publishers July 30, 2019
SHARE THIS:
Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akiongea na Makamu wa Rais wa Tuzo za Hollywood and African Prestigious (HAPA), Amberr Washington, ofisini kwake alipotembelea makao makuu ya Global Group yaliyoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam.
MAKAMU wa Rais wa Tuzo za Hollywood and African Prestigious (HAPA) kutoka Marekani, Amberr Washington, ametua ndani ya mjengo wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar na kueleza namna walivyojipanga kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji mbalimbali nchini Tanzania.
Amber amewapongeza wafanyakazi wa Global Group kwa namna walivyompokea na jinsi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Mmarekani huyo mwenye asili ya Afrika, alikuwa ameongozana na Balozi wa Tuzo hizo nchini ambaye pia ni mmiliki wa Master Tanzania, Mawini Casy, na mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda, Ofisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Henry Mrutu na ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Godffrey Nago.
Abdallah Mrisho akiwa na Amberr Washington na Balozi wa HAPA nchini Tanzania, Mawini Casy.Amberr akikabidhiwa Gazeti la Ijuma Wikienda na Mhariri wa Gazeti hilo, Sifael Paul. Wa pili kulia ni Meneja wa +255 Global Radio, Bori Mbaraka na kulia ni Mawini Casy ambapo Mhariri wa Global TV, Nyalobi Kelvin. anaonekana kwa nyuma. Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (katikati) akiwa na Amberr baada ya kufika ofisini kwake. Wa pili kulia ni Ofisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Henry Mrutu,akifuatiwa na Mawini Casy, na kushoto ni Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Godfrey Nago.Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda akiwa na Amberrwalipofika ofisi za Global Group.