
BAADA ya Yanga kuwasili Zanzibar na kuweka kambi ya muda mfupi kuelekea mchezo wao wa kimataifa, kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa hana presha na anaamini kufi kia Jumamosi watakuwa tayari kuwavaa wapinzani wao Township Rollers ya Botswana.
Yanga wanatarajia kuvaana na Township Jumamosi ijayo, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga mara ya mwisho kwenye Ligi ya Mabingwa ilicheza na Township Rollers msimu wa 2017/2018 na ikatolewa na kujikuta ikiangukia Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera alisema kuwa anaamini mapungufu ambayo aliyabaini katika kikosi chake anayafanyia kazi, hivyo kufi kia siku ya mchezo wao wa kimataifa wa keshokutwa Jumamosi kikosi kitakuwa sawa.

“Kuna vitu havikuwa sawa lakini kufi ka Jumamosi tunapocheza na Township ninaamini tutakuwa sawa kwa sababu timu inahitaji umakini na kufanya vizuri tukiwa hapa nyumbani.
“Na ukiangalia kikosi changu kuna maeneo yanatakiwa kufanyiwa kazi zaidi ili kuwa bora kwa mechi zilizopo mbele yetu,” alisema Zahera.