×

Utabiri Mwaka 2069: Nyumba za Kujifagia, Maghorofa ya Chini ya Ardhi!

WATAALAM wametabiri kwamba baada ya miaka 50 ijayo, kwenye mwaka 2069, dunia itakuwa imebadilika sana kisayansi, ikiwa ni pamoja na nyumba za makazi kujisafisha kwa mashine za roboti, kuweko maghorofa marefu chini ya ardhi, hoteli zinazoelea angani, teksi zinazopaa, njia za usafiri ndani ya maji, na kadhalika.

Utabiri unaonyesha kuwepo maghorofa marefu ya chini ya ardhi ambamo watu wataishi na kufanya kazi.

Ifikapo mwaka 2069, Waingereza watakuwa wakitembelea hoteli zilizo anga za juu wakati wa majira ya joto. 

Kampuni ya Samsung imesema patakuwa na teksi zenye kupaa mijini.

Njia za baharini zitaunganisha usafiri kwa muda mfupi kati ya Uingereza na nchi za  Scandinavia.

Michezo mbalimbali itakuwa inachezwa angani mbele ya watazamaji kwenye viwanja vya michezo.

Nyakati za mapumziko binadamu atakuwa anafungasha mabegi kwenda kwenye hoteli zilizo anga za juu.