WATU 40 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kuzuia na kushambulia msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya hiyo uliokuwa ukiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Cloudia Kitta.
Tukio hilo limetokea mapema juzi katika kijiji cha Mpunguti kata ya Makwale Wilaya ya kyela ambapo Mwenyekiti wa kamatai ya ulinzi na usalama huyo ameitisha kikao cha dharula na kutoa tamko kulaani shambulizi hilo.