×

Nywele Halisi za George Washington Zapigwa Mnada

KITITA  cha nywele za aliyekuwa rais wa Marekani, George Washington, ambacho kilikatwa na ndugu yake wakati akingali rais mwaka 1790, kinategemewa kuuzwa kwa zaidi ya Dola 50,000 (Sh. 114.8).  Nywele hizo zilihifadhiwa kwa hati maalum iliyoandikwa kwa mkono mwaka 1889.

Hati hiyo inasema:

Kitita hiki cha nywele kimekatwa kutoka kichwa cha George Washington, mnamo mwaka 1790, na ndugu yake.  Kitita kicho kilitolewa kwa Keptani Samuel Butman wa Newburyport, Wilaya ya Essex, Massachussetts: mtu ambaye alisafiri naye mara kadhaa kutoka Alexandria, Virginia kwenda bandari ya Newburyport.

This lock of hair was cut from the head of George Washington, about the year 1790, by a relative of his. It was presented by this same relative to Capt. Samuel Butman of Newburyport, Essex County, Massachusetts; with whom the aforesaid relative made several trips from Alexandria, Va, to the port of Newburyport.

Photo Credit: TMZ