×

Rais Museveni Kuwasili Nchini Kesho

RAIS  wa Uganda, Yoweri Museveni, anatajiwa kuwasili kesho nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Septemba 5 hadi 7, 2019, ambapo atapokelewa na mwenyeji wake, Rais John Magufuli .

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Museveni atawasili saa 12.00 jioni ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda, na pia anatarajiwa kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam siku ya Septemba 6, 2019.

Kuhusu kuachiwa kwa ndege ya ATCL fungua video hapo chini.