WANANCHI mkoani Geita, kijiji cha Kasala kata ya Makulugusi wilayani Chato hivi majuzi wakijikita katika kile walichokiita baraka kwa kumpa nyoka chatu (mnyama) mbuzi na vitu kadhaa kama sadaka ili kufanikisha mwenendo wa maisha mema hapo kijijini.
Nyoka huyo anayedaiwa alionenakana hapo, wazee wa kijiji hicho walitaka apewe vitu hivyo vikiwa ni sadaka.
Mzee Isaka Wandiba Nyamkura wa kjiji cha Mugusu amesema kukosekana kwa mavuno na uwepo wa magonjwa mengi ni kichocheo kikubwa cha wao kufika hapo na kuomba kwa kumpa nyoka huyo vitu hivo ili aweze kuwasaidia.
Alisema kijijini hapo mwaka 1997 alitokea nyoka mkubwa wa namna hiyo na wazee walikusanyika na kumpelekea mbuzi, hali iliyosababisha kutokea kwa neema kubwa ya mvua.
Naye Philipo Lazaro mkazi wa kijiji hicho anasema miaka minne iliyopita aliwahi kutokea nyoka wa namna hiyo kijiji hapo ambapo wananchi walimpiga na kumuua lakini baadaye walipata madhara makubwa.
Tangu kutokea kwa nyoka huyo kijiji hicho kumekuwa na wageni wengi kama wanavyobainisha wakazi wa kijiji hicho na mwenyekiti kijijini hapo akikiri kutokuwepo kwa madhara yoyote kutokana na uwepo wa nyoka huyo.