×

Nandy Alivyotapika Kwenye Lifti!

MWANADADA mkali kwenye Bongo Fleva kwa sasa, Faustine Charles Mfinanga ‘Nandy’ ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yaliyowahi kumtia aibu ni kitendo cha kutapika kwenye lifti.

Akizungumza na redio moja jijini Nairobi, Kenya wikiendi iliyopita, Nandy alisema ishu hiyo ilimtokea kwenye jengo moja refu mjini akiwa na mpigapicha wake wakiwa wawili tu kwenye lifti hiyo.

Nandy alisema lifti ilipofika kwenye floo ikasimama wakaingia watu wengine, alijifanya aliyefanya tukio hilo ni mpiga picha wake.

 

“Tulikuwa kwenye lifti, tulikuwa wawili tu, mimi na mpiga picha wangu, nilikuwa na tatizo la tumbo.

“Nilitapika, lakini ndani ya muda mfupi lifti ilisimama, wakaingia watu wengine,” alisema Nandy.

“Wakati watu hao wanaingia, bado kulikuwa na harufu kali kwenye lifti na ili kuua soo, ilibidi nijifanye kumlaumu mpiga picha wangu, nilijidai kumuuliza kwa nini unatapika..,” alisema Nandy na kuangua kicheko kizito.

 

Baadaye aliendelea na mahojiano huku akisisitiza kuwa yeye siyo mjamzito kama ambavyo kurasa nyingi za udaku za Instagram zimeendelea kusambaza taarifa hizo.