
NCHI ya China imezindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing, ambao ni mkubwa zaidi duniani ambao umegharimu zaidi dola bilioni 11 (Tsh trilioni 25.3).

Uwanja huo uliopo mjini Beijing ulizinduliwa rasmi na rais Xi Jinping, una ukubwa wa mita 700,000 mraba na wenye ukubwa wa sawa na viwanja vya mpira 98.

Ukikamilika wote mwaka 2025 (ukiwa na njia nne za ndege kurukia) utahudumia abiria milioni 72 kwa mwaka.
Uwanja huo uliopatiwa jina la Daxing unauwezo wakuingiza abiria wengi zaidi kwenye jengo moja na kupokea wasafiri zaidi milioni 170.
Mtandao wa kiserikali, Global Times umeripoti kuwa ndenge saba zinatarajiwa kuanza shughuli katika uwanja huo mpya.