×

Mapya Yaibuka Sakata la Griezmann

Antoine Griezmann

MAMBO mapya yameibuka kuhusiana na sakata la Antoine Griezmann kujiunga na Barcelona.

Atletico Madrid imelalamikia kitendo cha Griezmann kusajiliwa na Barcelona wanaotuhumiwa kukiuka kanuni za usajili.

 

 

Klabu hiyo inashikilia kuwa Barcelona walishamalizana na Griezmann kabla ya kuwasiliana na klabu hiyo.

Griezmann imebainika kuwa kumbe alivuta kiasi cha Euro milioni 14 (Sh. bilioni 35) kama kamisheni ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Barcelona.

 

 

Mwanasheria wa Griezmann inasemekana ndio alifanya mawasiliano na Barcelona kuhusu pesa hizo na kuzidi kuthibitisha kumbe Barcelona walishamalizana na staa huyo tangu Machi mwaka huu kwa mujibu wa gazeti la El Mundo.

 

Atlético Madrid wanataka walipwe kiasi cha euro milioni 200 (Sh. bilioni 506) badala ya euro milioni 120 (Sh. bilioni 303) walizolipa Barcelona.

 

Barcelona ililipa fedha hizo ikitumia mwanya wa mkataba wa Griezmann na Atletico ulioelekeza klabu inayomtaka staa huyo ingeweza kulipa kiasi cha euro milioni 120 kuanzia Julai mwaka huu.

 

Mwanasheria wa kifaransa ndio alikuwa anafanya mawasiliano hayo na Barcelona inadaiwa walitoa fedha hiyo kwa baba, dada na wakala mmoja wa kifaransa kukamilisha dili hilo.

 

Kuna uwezekano mkubwa kwa Barcelona kuadhibiwa kufuatia kitendo hicho cha kutuhumiwa kumsajili Griezmann kinyume cha taratibu.

DULLA MBABE Kunogesha Pambano la USIKU wa MABINGWA