×

BONGO STAR SEARCH YAREJEA KWA KISHINDO

LILE Shindano maarufu la kusaka vipaji la Bongo Star Search 2019 limeibuka kwa kishindo cha aina yake, wanakwambia shiriki uwe star.

Bongo Star Search ni kipindi cha kusaka vipaji kupitia Televisheni.

Kipindi hiki kimelenga kumtafuta muimbaji mahiri kupitia usaili utakaofanyika mikoa mitano hapa Tanzania.

 

Watazamaji pia watashiriki kwenye mashindano na kumchagua mshindi kwa kupiga kura mtandaoni.

BSS 2019 inatoa fursa msimu huu wa 10 ya kutafuta vipaji mahiri vya vijana machachari wa Kitanzania.

BSS 2019 inaletwa kwenu na StarTimes na itarushwa kwenye Chaneli ya StarTimes Swahili na APP ya StarTimes ON.

 

Bongo Star Search wanawakaribisha wale wote wenye vipaji kushiriki usaili kwenye mikoa husika na kwenye mtandao kupitia App ya StarTimes ON.

Usaili utaanza Septemba 28, mwaka huu katika mikoa 5 kama ifuatavyo:

Septemba 28 & 29– Arusha (Fuzz-Pointzone Resort -Mianzini)

Oktoba 4 & 5 – Mwanza (Rock City Mall)

Oktoba 10 & 11– Mbeya (Mbeya City Pub & Lounge)

Oktoba 17 & 18- Dodoma (Royal Village Hotel)

Oktoba 23, 24 & 25 – Dar es Salaam (National Museum).

Kutakua na majaji mahiri wanne watakaotoa kura za NDIO au HAPANA kwa washiriki baada ya kuangalia umahiri wao katika kuimba.

Ukipata kura tatu za NDIO moja kwa moja utakua umeshinda kuingia mchuano wa pili, ukipata kura mbili za NDIYO utasonga mbele.

 

Usaili wa mtandaoni utafanyika kuanzia Oktoba 8 mpaka 30. Kwa kushiriki unaweza ukajaza fomu kupitia Application ya StarTimes ON kisha weka Link kwenye YouTube au jirekodi kisha post Instagram na kuweka hashtag #bssonline,

www.startimestv.com, audition2019 na @startimestz.

 

Tuma walau wimbo uliokamilika na urekodi mwingine bila kuhariri (edit) na kurudiarudia. Muimbaji aonekane kabisa akiwa anajirekodi na pia inatakiwa muimbaji aonyeshe hisia akiwa anaimba na kucheza.

Mchujo utafanyika ndani ya saa 48 na majibu yatatangazwa katika kurasa za Bongo Star Search na StarTimes.

 

Mwisho wa upigaji kura washindi wa 30 wa mwanzo wataingia kwenye mchuano.

Usaili wa Bongo Star Search utarushwa hewani kuanzia tarehe 13 Oktoba kila Jumapili saa mbili kamili kupitia Chaneli ya ST Swahili. Usiache kushiriki kwani nani ajuaye! Star wa kesho anaweza kua ni wewe.

 

StarTimes ni Televisheni ya Kidigitali inayoongoza barani Afrika, ina watumiaji takriban milioni 28 na imesambaa barani kote Afrika pamoja na idadi kubwa ya mtandao wa wasambazaji takriban 170, pamoja na hiyo StarTimes ina chaneli 480 zilizoidhinishwa ikiwa ni pamoja na habari, series, michezo, burudani, vipindi vya watoto na kadhalika.

 

Lengo la kampuni ni kuhakikisha kila familia ya Kiafrika inaweza kumudu, kupata na kufurahia televisheni kidijitali.

Stori:Neema Adrian, Global Publishers