
OPARESHENI za kuopoa miili ya mama na mwanaye waliozama siku ya Septemba 29, 2019, katika feri ya Likoni, Mombasa, Kenya, zinaendelea kwa vikosi vya serikali, sekta binafsi na kutoka Afrika Kusini vikishirikiana.
Uwepo wa vikosi vya wazamiaji wa Afrika Kusini umeongeza nguvu lakini kina cha bahari, vifaa visivyo na ubora pamoja na uonaji usio mzuri ni changamoto kubwa katika uokoaji huo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa huduma katika feri hiyo, timu ya wazamiaji kwa sasa itategemea zaidi teknolojia kusaidia kutambua vitu chini ya bahari na kupata mwili wa Mariam Kighenda (35) na mwanaye (4)
Mariam na mwanaye wazama baharini na kuaminika kufa baada gari lao kuteleza kutoka kwenye kivuko wakati wakivuka katika kivuko cha MV Harambee kilipokuwa kinakaribia kuwasili kisiwani Mombasa.
Chanzo:Jamii forum