×

Hasheem: Nimeishi na Unga Tumboni Miezi 2 – Video

HUU ni Ushuhuda wa Hasheem Hasheem mzungu aliyeangukia kwenye dimbwi la usafirishaji wa dawa za kulevya na baadaye akawa teja.

 

Moja ya vitu vya kutisha alivyowahi kuvifanya ni pamoja na kukaa na dawa za kulevya kwa siku hamsini na saba tumboni.

 

Kijana huyu amepitia changamoto mbalimbali katika safari yake ya maisha ikiwa pamoja na kutengwa na familia yake kutokana na vitendo alivyokuwa akivifanya akiwa teja. Licha ya yote aliyoyapitia kijana huyu ameamua kuitumia safari ya maisha yake kuwa funzo kwa vijana wenzake.