
BOSI wa Pyramids ya nchini Misri ametua jijini Mwanza jana pamoja na baadhi ya wajumbe wa timu hiyo kwa lengo la kuweka mambo sawa kabla ya kikosi chao kutua kesho Ijumaa. Yanga inamenyana na Pyramids katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili hii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Rogers Gumbo amesema kuwa, wageni wao Pyramids wameshatua jijini Mwanza kwa upande wa mratibu wa timu hiyo pamoja na baadhi ya wajumbe kwa ajili ya kuwka mambo sawakabla ya kikosi kamili kutua kesho.

“Wametuambia kuwa watakuwa na msafara wa watu 32 ila hawajatueleza wachezaji watakuwa wangapi na viongozi na benchi la ufundi wangapi,”alisema Gumbo. 10:00 Yanga inacheza na Pyramids Jumapili saa 10:00 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba