×

Mzee Pinda, Mwakyembe Wahudhuria Kongamano la Wanawake Wajasiriamali

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni   Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto), pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia), akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam.