×

Angalia Mpoki Alivyochagiza Uzinduzi Wa Smart Kitochi

Lugeta (kushoto) akiwaonesha (wanahabari hawapo pichani) bango linaloonesha maelekezo ya simu hiyo.

Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom jana ilizindua simu mpya inayokwenda kwa jina la Smarti Kitochi. Akizungumza na wanahabari kwenye duka la Vocacom Mlimani City Dar, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Mawasiliano wa kampuni hiyo, George Lugeta amesema simu hiyo wameipa jina hilo kutokana na uwezo wake mkubwa unaofanana na smart phone. Lugata amesema simu hiyo ina spidi ya aina yake katika matumizi ya data ikiwa Whatsapp, Facebook, Twitter, na mitandao mingine.

Mmoja wa wateja aliyenunua simu hiyo kwenye uzinduzi huo akiijaribu.
Msanii wa komedi, maarufu kwa jina la Mpoki (kulia) akichagiza kwa vichekesho wakati akimpongeza mteja aliyenunua simu kwenye uzinduzi huo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/GPL