×

Odemba ajitoa kimasomaso!

MWANAMITINDO wa kimataifa Bongo mwenye makazi yake jijini Paris, Ufaransa, Miriam Odemba amejitoa kimasomaso katika kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama huko Mkuranga, Pwani.  Odemba ni Balozi wa Shirika la African Reflection Foundation chini ya Balozi wa Heshima wa Visiwa vya Shelisheli (Seychelles), Marry Vonne.

Huko Mkuranga, mbali na kuhamasisha upatikanaji wa maji safi, pia amewatengenezea akina mama mazingira ya sehemu kubwa ya kupanda mbogamboga (green house).

Odemba ameliambia Gazeti la Ijumaa; “Ndoto yangu ni kuona Watanzania wenzangu hasa akina mama wanaweza kujikwamua kwenye maisha yao ya kila siku.

Stori: Imelda Mtema, Dar