×

Rais JPM Amwapisha CAG Mpya, Majaji 12

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bw. Charles Edward Kichere mara baada ya kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4, 2019

 

Rais Magufuli akimuapisha Bw. Joachim Charles Tiganga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Deo John Nangela kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Bi. Angela Anthony Bahati kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 4, 2019

 

Rais Magufuli akimuapisha Bw. Angaza Elias Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu Kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Bi. Amina Talib Ali Kuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Mhandisi Aisha Amour kuwa balozi wa Tanzania Nchni Kuwait. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019.

 

Rais Magufuli akimuapisha Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 4, 2019.

 

Viongozi walioapishwa na Rais Magufuli wakila kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019.

 

 

Rais Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha CAG, Majaji 12 wa Mahakama Kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam novemba 4, 2019.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha Dkt. Isidori Mpango pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam novemba 4, 2019.
Rais Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, CAG, Charles Kichere, Watendaji wa Ofisi ya CAG pamoja na Makamu mwenyeki wa Kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Aesh Hilaly Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4, 2019. PICHA NA IKULU