

Wateja zaidi ya milioni 14 wa Vodacom watanufaika na huduma ya malipo kwa M-Pesa kwenda halmashauri na manispaa mbalimbali nchini Tanzania.
Kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI wamefanikisha kuimarisha mfumo wa malipo ya kifedha kwa kusogeza huduma ya malipo kwa M-Pesa kwa ofisi zaidi ya ofisi 127 za Serikali za Mitaa nchini.
Uzinduzi wa huduma hiyo, ulifanyika ofisi za Makao Makuu ya Vodacom, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo.
Na Neema Adrian