×

TACAIDS Waipongeza Kampuni ya Cool Blue

Mkurugenzi Mtedaji wa TACAIDS, Dkt. Leonrad Maboko (kulia) akiongea na wanahabari akiwa na Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano cha  TACAIDS Nadhifa Omary.

TUME ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) leo Novemba 6, 2019 imetembelea Kampuni ya maji safi ya Cool Blue Mikocheni jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kuwafanya watu wajiepushe na kuwa waangalifu kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi na kuiona kampuni hiyo ni moja katika mapambano ya kudhibiti Ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya maji safi ya Cool Blue, Fauzia Malik (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Muitikio wa Kitaifa, Odri Njeleka.

Mkurugenzi Mtedaji wa TACAIDS, Dkt. Leonrad Maboko, alisema kuwa ameuona mchango wao wa muda mrefu sana kupitia karatasi lililo kwenye maji hayo, ambao ni muhimu sana kuwakumbusha watu kuhusiana na Ugonjwa huo na ndio maana waliwatembea kwaajili ya kuwapa motisha zaidi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya maji safi ya Cool Blue, Fauzia Malik ameipongeza TACAIDS kwa kutambua mchango wao wa kutoa elimu ya Ukimwi kupitia maji yao ya Cool Blue na wataendelea kuelimisha jamii.

…Dkt. Leonrad Maboko akiendelea kuongea jambo.
Mkurugenzi wa Utawala TACAIDS, Yasini Abbasi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa sera na Mipango wa TACAIDS, Richard Ngilwa (katikati) na  Mmoja wa wakurugenzi wa Cool Blue Sophia Maliki.

    HABARI NA IMELDA MTEMA | GPL