×

T-Bway: Siwezi kumuacha Kim Nana

KUTOKANA na habari kuzagaa kwamba wamemwagana, mtangazaji wa Kipindi cha 5select kinachorushwa na runinga ya East Afrika, T-Bway ameibuka na kusema hawezi kumuacha Kim Nana kamwe kwani anampenda sana.

Akichonga na Kipindi cha Funk Friday kinachorushwa na Global Radio, T-Bway alisema maneno yanayozungumzwa ni mengi lakini hayana ukweli wowote kwani na yeye na mpenzi wake, Kim Nana wako pamoja na hawajaachana.

“Habari za kwamba nimeachana na Kim Nana nazisikia kwenye mitandao kitu ambacho siyo kweli, watu wameamua kuchafua uhusiano wetu, nawaomba wale wanaoandika mitandaoni wawe makini maana ipo siku hizo habari za kizushi zitawaponza wataenda jela,” alisema T-Bway.

 

Stori: KHADIJA BAKARI