×

Wateja watano Wajishindia Bodaboda na Ibuka Kidedea na NBC Malengo

Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam  wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni  ya akaunti ya Malengo ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya bodaboda  kila mmoja.  
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (mbele kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam  wakati  NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni  ya akaunti ya Malengo ya NBC ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya pikipiki aina ya Yamaha kila mmoja.  Washindi wa  ni;  Augustine Hatari kutoka Pwani, Williumu Pendaeli Isack wa Moshi,  Scholastica Peter Yamawasa, Honest Christopher Kimaro na  Daudi Majani wote kutoka Dar es Salaam.