×

INFINIX YAZINDUA INFINIX S5 KWA KISHINDO

Kampuni ya Infinix imezindua rasmi simu kali, toleo jipya aina ya Infinix S5. Uzinduzi huo umefanyika mapema leo katika Duka la Infinix lilipo Mlimani City jijini Dar. Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Infinix, Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Infinix, Aisha Karupa amesema Infinix ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali na kuwahakikishia wateja kupata bidhaa hizo zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei rafiki.

“Sifa ambazo zinapatikana kwenye simu hii ni pamoja na kuwa na selfie kali yenye 32MP, lakini ina sifa lukuki kama vile teknolojia ya Artificial Intelligence yenye kamera 4 za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens. “Pia Infinix ina memory card ya ziada ya ukubwa wa GB 4 kwa GB 64 yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi bila kuhitaji memory card za ziada.

“Infinix S5 imekuja ikiwa kwenye mwonekano wa kitofauti wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya display kwa jina la kitaalam ikijulikana kama Infinity-O Display kwa wale wenye matumizi mengi. “Infinix S5 ina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kutokana na ujazo mkubwa wa battery wenye mAh40,000,” alisema.

Pia Infinix wametumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi promosheni ya msimu wa sikukuu inayokwenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5 ambapo meneja mauzo wa Infinix, Fredy Kadilana alisema, katika msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

“Promosheni hiyo itampa nafasi mteja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na nyingine nyingi bila kusahau wadau wake wanaotembelea kurasa 2@infinixmobiletz kwa kuitambulisha challange ya #S4showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii,” alisema.