FAMILIA ya marehemu Rashid Mfaume Kawawa inasikitika kutangaza kifo cha kaka yao mkubwa, Alhaji Mfaume Rashid Kawawa, kilichotokea leo Jumatatu, Januari 27, 2020, Madale jijini Dar es Salaam.
Msiba upo Madale kwa mzee Kawawa na mazishi yatafanyika kesho Jumanne alasiri hapohapo Madale kwa mzee Kawawa.
=======================================
Marehemu mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika na mpigania uhuru wa Tanganyika na Muasisi wa Muungano ambaye alifariki dunia Desemba 31, 2009 (akiwa na umri wa miaka 83).
Mzee Kawawa alikuwa ni swahiba wa karibu zaidi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, na ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Awamu ya Kwanza wa Serikali chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
INNALILAH WAINNAILAIH RAJIUN!