
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungnao wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu, Januari 28, 2020, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri huyo leo wakati Mhe. Zungu alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kupokea maelekezo mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa Majukumu yake.

Aidha, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtakia Waziri Zungu kila la heri katika utendaji wa Majukumu yake na amemtaka afanye kazi kwa bidii na Spidi zaidi.

View this post on Instagram