×

JPM: Maendeleo Hayateremki Kama Mvua – Video

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewaahidi wananchi wa Manyoni mkoani Singida  kuendelea kuwaletea maendeleo iwapo watamchagua tena katika kipindi cha miaka mingine mitano.
Magufuli amesema hayo leo, Septemba 1, 2020 akiwa katika kampeni zake za urais wakati akielekea Singida Mjini anakotarajia kufanya mkutano mkubwa baadaye leo.

“Maendeleo hayateremki kama mvua, hata corona tumeiondoa kwa kusali, angalieni nchi zingine kila siku wamejifunga midomoni, hata mke wako unaweza ukamsahau, unaweza usimjue kama ni mwanamke au mwanaume kwa sababu hawakumtangulliza Mungu.

 

“Ninaomba kura kwa Watanzania wa vyama vyote, maendeleo hayana chama, mnichagulie wabunge ambao wataleta taarifa kwenye makao makuu, wabunge ambao hawaliogopi bunge na huwa hawakimbii bungeni na wanakaa kwa ajili ya kuomba miradi ya Watanzania,” alisema.

 

 

Leave a Comment