MSANII wa Bongo Fleva, Maua Sama, amefunguka kuwa mpaka sasa bado hajapata muda wa kuitazama ngoma mpya ya msanii nguli wa muziki duniani, mwanadada Alicia Keys kutoka nchini Marekani ambayo amemshirikisha supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz iitwayo ‘Wasted Energy’ kutokana na kutopkana na kile alichodai kuwa amekuwa bize kwa muda mrefu.
Maua amesema hayo leo Alhamisi, Oktoba 1, 2020, wakati akipiga stori na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio.
“Sijasikiliza wimbo mpya wa Alicia Keys na Diamond ‘Wasted Energy’ sababu nimekuwa bize kusafiri na vitu vingine kwa muda, nimeona tiza tu, ila nimesikia amefanya hiyo kolabo, ni kitu ambacho wasanii tunahitaji kufanya international kolabo kubwa.
“Ninaandaa vitu vyangu by next month tutaanza kuachia, hapo nyuma kulikuwa na corona na sasa ni uchaguzi, kwa hiyo vimekwamisha mambo mengi, kulikuwa na albums, EPs ambazo zinahitaji international collaborations, lakini lockdown imeharibu, kwa sasa tunasubiri muda tu.
“Kufanya shows kwenye majukwaa ya siasa imenisaidia ku-gain vitu vipya, kuwa karibu na mashabiki na kuonyesha mazuri ambayo Rais wetu, Dkt. Magufuli ameyafanya kwa Taifa letu. Najua kuna wasanii wengi Afrika Mashariki lakini nashukuru kuchaguliwa kuwania Tuzo za AFRIMA, hili ni jambo kubwa sana kwangu.
“Nimeimba sana nyimbo za Jide Jaydee kabla sijatoka kimziki, ni msanii mzuri na kila msanii mwanamke anatamani kuwa kama yeye, nitafurahi siku moja nikitimiza ndoto yangu ya kupata Tuzo ya Grammy, itanisaidia kunipaisha kimataifa,” amesema Maua Sama.

