RAIS wa Jamuhuri ya Muunguno wa Tanzania John Magufuli hii leo amepokea gawio la Sh Bilion 100 kutoka Kampuni ya Madini ya Twiga inayomilikiwa kwa ubia na Kampuni ya Barrick Gold Mine na Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Serikali imepokea gawio la shilingi bilioni 100 kutoka Kampuni ya Twiga na shilingi bilioni 1.1 kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
“Makubaliano haya yanaleta faida kwa Watanzania wanaoachiwa mashimo na umasikini wa mali walizoachiwa na Mungu wao ikichukuliwa na kusombwa na watu wengine.”
“Nawashukuru timu ya maridhiano, chini ya Prof. Kabuni, Gavana na wengine, hawa ndio wamefanya tupate hizi fedha, sababu ya unyeti wa mazungumzo ilibidi wakati mwingine walale ofisini, wanakesha wakizungumza, saa nyingine tuliwafungia wasirubuniwe na matajiri.
“Kupatikana kwa hizi Bilioni 100, nafahamu kama ni uwekezaji wa matrilioni ya pesa, nyie mna 84% sisi tuna 16% pekee, lakini faida tunagawana 50% kwa 50%, na ndiyo tumeanza, najua mtakapopiga mahesabu vizuri zitakuwa nyingi zaidi, naomba na zenyewe zije haraka.
“Fedha hizi tunazozipata zitatusaidia kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya afya, miundombinu, elimu n.k, tunawashukuru sana Kampuni ya Barrick kwani makubaliano kati ya Kampuni hiyo na Serikali yetu yanaleta tija nchini.
“Ninawakaribisha wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza hapa nchini, Serikali yangu haiwachukii wawekezaji inawapenda, ndio maana tuliingia mazungumzo na kampuni kubwa ya kimataifa ya Barrick, ninaamini watakuwa mabalozi wetu kwamba Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza.
“Tunataka wawekezaji wakija iwe ni win-win situation, tusiachiwie mashimo tu, tunataka tufanidi rasimilami zetu, tunakarinisha makampuni mengine yaje yachimbe helium, gesi, mafuta, dhahabu na madini mengine, hata nyie maaskofu au mashehe huzuiliwi kuwa na kitalu chako.
“Tunataka kufanya biashara, tunataka tuwe na mabilionea wa nje na wa Tanzania kama Laizer, huyu mtani wangu ni Mmasai nilikuwa sijawahi kumuona, ndio maana nilitoa ahadi aje nimtafutie na mke wa Kisukuma huenda na sisi tutapatapata, hii ndiyo Tanzania nayoitaka.
“Nitafurahi siku moja nikienda mkoani nikakuta Mgodi wa kakobe unaitwa Kakobe Minerals au Mzee wa Upako Minerals au Gamanywa Minerals, hakuna ubaya, sisi ni matajiri sana, kila mahali kuna madini, kila mahali kuna pesa.
“Nilishaozoea kuambiwa nazungumza yasiyowezekana baadaye yanawezekana, nilisema tutajenga barabara kutoka Mtwara mpaka Bukoba watu watakwenda hata kwa Tax, wakaniambia huyu anaota ndoto za mchana lakini tulifanikiwa na leo watu wanapita hata kwa bajaji.
“Nikasema jamani #Corona tukimtanguliza Mungu itaisha, wakasema imewashinda Wazungu wewe ndiyo uizuie, lakini Mungu alitusikiliza, kuna rais mmoja aliniambia Mungu yuko bize hawezi kukulikiliza wewe tu, sasa juzi nikakutana naye mahali akaniambia mshukuru Mungu.
“Taifa hili Mungu amelipenda, lazima ifike mahali watu wakubali ukweli, tuliambiwa tutaoota watu wanakufa, maiti zinaokotwa barabarani, Mungu hajaenda likizo, yupo na anamsikiliza yule anayemuomba, ndiyo maana nawashukuru viongozi wa dini na Watanzania kwa maombi.”
“Siogopi kuwa sadaka ya Watanzania, kwa sababu huu ni wajibu wangu wa kuwasemea Watazania, kwani katika kipindi hiki hawana rais mwingine bali mimi mpaka atakapokuja mwingine, wameonewa mno, nataka Watanzania watajirike, nataka mabilionea wengi kama Laizer.
“Mnamuona Laizer mwenyewe licha ya kuwa bilionea lakini hajabalidilisha chochote, hana complication yoyote, ndio Utanzania huo, ameni-inspire sana, na matajiri wengi hawana compilications,” amesema Rais Magufuli.
