
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis (84) amepewa dosi ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya corona iitwayo Pfizer jijini Vatican jana Jumatano.
Papa huyo amepewa kinga hiyo licha ya kuwa na pafu moja baada ya jingine kufanyiwa upasuaji na kuondolewa wakati akiwa mdogo kutokana na matatizo mbalimbali.

Aidha, aliyewahi kuwa kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo duniani, Papa Mstaafu, Emeritus Benedict (93), naye amepewa chanjo hiyo leo ambapo wote wawili wanatarajiwa kupewa tena awamu ya pili ya chanjo hiyo baada ya wiki tatu zijazo.
Imeelezwa kuwa wakati wa utoaji kinga hizo, taratibu zote za kuwalinda wahudumu na viongozi hao waandamizi wa kanisa sambamba na wasaidizi wao, zilikuwa zimezingatiwa.
Mpaka sasa, watu 27 wameshathibitishwa kukutwa na Corona jijini Vatican ambapo 11 kati yao ni walinzi (wasaidizi) wa Vatican.