
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amewateua wasanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Nandy, Harmonize, Idris Sultan, Monalisa na wangangazaji Oliver Nyeriga wa Eatv, Millarda Ayo wa Clouds Fm na Masoud Kipanya kuwa Mabalozi wa Uhamasishaji Utunzaji wa Mazingira nchini.
Jafo amewateuwa wasanii hao akiwa Jijini Dodoma na kusema Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na ushawishi wao kwa jamii ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti.
Aidha, mabalozi wengine walioteuliwa na Jafo ni Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, Mbunge Esther Matiko, Mbunge Joseph Musukuma, Sakina Abdulmasoud, mchekeshaji Mai Zumo, Antonio Nugaz. Wengine ni wabunge, Eric Shigongo, Esther Matiko na Joseph Kasheku ‘Musukuma’.