×

Tajiri Aliyejijengea Kaburi la Bilioni 1 Akafariki, Mtoto Asimulia Mzito – Video

Takribani miaka minne iliyopita, mwaka 2018, tukio lisilo la kawaida lilivipamba vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi! Lilikuwa ni tukio la mganga wa jadi, Anthony Lumuliko Mwinami almaarufu Dokta Mwandulami, mkazi wa Kijiji cha Wangama, Kata ya Mtwango mkoani Njombe kuzungumzia kuhusu ujenzi wa kaburi ambalo mwenyewe alitaka atakapofikwa na mauti, azikwe hapo!

 

Kwa mujibu wa maelezo yake, Mwandulami alieleza kwamba ameamua kujenga kaburi hilo lenye ghorofa moja na urefu wa mita 12 kwenda chini, sehemu ya mapumziko pamoja na sehemu watakapozikwa wake zake watatu, ili watakapozikwa, kumbukumbu zake ziendelee kubakia vizazi na vizazi, kwa sababu kazi aliyokuwa anaifanya kwa jamii, ilikuwa kubwa na inayohitaji kuenziwa. Si yeye pekee aliyepanga kuzikwa kwenye kaburi hilo, bali pia, wake zake watatu!

 

Waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari, vya ndani na nje ya nchi, walifunga safari mpaka katika kijiji hicho, kujionea kilichokuwa kinaendelea kwa sababu si kawaida kwa watu wengi kujiandalia makaburi ambayo watazikwa watakapofikwa na umauti.

 

Leave a Comment