
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021.
Jengo hilo lililogharimu TZS bilioni 9 ni moja ya majengo matano yaliyojengwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam (2).
Majengo ya Vituo sita Jumuishi vya Utoaji Haki yatakuwa na mahakama za ngazi zote. Kesi ikimalizika katika ngazi moja, mhusika asiporidhika, atakata rufaa katika mahakama ya juu iliyopo kwenye jengo hilo hilo.