×

Mbunge Wa Zamani, Nimrod Mkono Afariki Dunia – Video

Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya Aprili 18, 2023 kwa saa za Marekani.

Akithibitisha kifo hicho Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amesema kaka yake aliondoka Nchini Tanzania tangu mwaka 2018 kwenda Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea

“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye” Amesema Zadock.

Leave a Comment