
Tume ya pamoja inayoshughulikia usuluhishi katika eneo lenye mgogoro la Sahara ya Magharibi, imeshauri kuwa mazungumzo ya Amani na majadiliano ya kisiasa, yatumike kusuluhisha mgogoro huo kwa faida ya nchi zote za ukanda huo.
Tamko la pamoja lililotolewa jijini Rabat katika mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Morocco na Angola limeunga mkono jitihada za Mjumbe Maalum wa Shirikala Umoja wa Mataifa, Staffan Mistura za kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa majadiliano.
Eneo la Sahara ya Magharibi, linagombaniwa na Serikali ya Morocco na Kundi la Polisario Front lenye makazi yake nchini Algeria ambapo kumekuwa na hofu ya kuibuka kwa mapigano baina ya pande hizo, kila upande ukidai kuwa eneo hilo ni lake.
Mkutano uliotoa tamko hilo, umewakutanisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Morroco, Nasser Bourita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Téte Antonio na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Staffan Mistura.
Mawaziri hao, kwa pamoja wameeleza kwamba kila nchi inayohusika na mgogoro huo, inapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za mipaka na kuheshimu uhuru na mamlaka ya nchi husika.