Benki ya Stanbic Tanzania imekabidhi msaada wa meza 20 kwa kituo cha watoto wanaoishi na ulemavu wa mtindio wa ubongo cha Sibusiso Foundation, cha jijini Arusha jana.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa Benki ya Stanbic kurudisha kwa jamii na kusaidia watoto hao waweze kupata elimu itakayowafanya waweze kujitegemea.

