
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kufuatia Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Mkutano chini ya uenyeji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hali ya usalama imeimarishwa mara dufu Februari 07, hadi 08, 2025 na baadhi ya barabara zitakuwa zinafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kupisha misafara ya Viongozi wa mkutano huo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema barabara ambazo zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kadri itakavyoruhusu ni barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.
