×

Wasira Asisitiza Uchaguzi Mkuu Utafanyika Kama Ulivyopangwa na NEC (Picha +Video)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wassira Akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza, Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ukumbi wa CCM KIRUMBA uliopo Wilaya ya Ilemela Mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utafanyika kama ulivyopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akizungumza Katik Mkutano wa Hadhara, 2025, jijini Mwanza Feb 10 2025 , Wasira alieleza kuwa hoja ya kutaka mabadiliko ya Katiba kabla ya uchaguzi huo imechelewa, hivyo uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na hakuna chama kinachoiweza kuzuia uchaguzi kwa kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria

Wasira alitoa wito kwa vyama vya siasa, hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na kuheshimu maridhiano yaliyopo badala ya kushikilia msimamo wa kutaka mabadiliko ya Katiba kabla ya uchaguzi.

Stephen Wassira, akisimikwa jina la ”NTAMBULWA” lenye maana ya Kiongozi Mkuu wa wazee ambapo alikabidhiwa Usinga wa Nyumbu alama ya Uongozi na uwezo wa kuita umati Mkubwa wa watu wakaitikia.