
Mahakama nchini Mauritius imemuachia kwa dhamana Waziri Mkuu wa zamani, Pravind Jugnauth aliyekamatwa jana Jumapili kwa tuhuma za rushwa na utakatishaji wa fedha haramu.
Baada ya kukamatwa na maafisa wa Kitengo cha Uchunguzi wa Tuhuma za Uhalifu wa Kiuchumi, walienda kufanya upekuzi kwenye nyumba yake na kumkuta akiwa na fedha kiasi cha rupia milioni 114 za Mauritius, sawa na takribani shilingi bilioni 6.5 za Tanzania.
Kiongozi huyo mstaafu anakuwa kigogo wa pili kukamatwa nchini Mauritius baada ya mwezi uliopita, Gavana Mstaafu wa Benki Kuu ya Mauritius, Harvesh Seegolam kukamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana.