
Elimu ya Ujuzi wa Fedha ya Benki ya Stanbic Tanzania inaendelea kuhimiza utoaji wa elimu ya fedha kupitia mpango wake wa kipekee unaolenga kuwapa familia stadi muhimu za usimamizi wa fedha.
Mpango huu unawalenga watoto kwa kuwaelimisha kuhusu jinsi ya kupata, kutumia, kuweka akiba, na kutoa pesa kwa uwajibikaji, huku ukiwaimarisha katika nidhamu ya kifedha tangu utotoni.
Kwa kushirikisha familia katika mbinu shirikishi na za kufurahisha za kujifunza, Benki ya Stanbic inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kujenga kizazi chenye uelewa mzuri wa masuala ya fedha na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yao ya baadaye.
Safari hii, utoaji wa elimu ya Ujuzi wa Fedha umefanyika katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza, ikiwa ni maalum kwa wateja wa huduma za Benki binafsi pamoja na familia zao.
Tukio hili liliwapa watoto wa wateja fursa ya kushiriki katika shughuli za kuvutia kama vile michezo ya bajeti, mazoezi ya uigizaji wa majukumu, na majadiliano ya kina kuhusu misingi ya fedha.
Kwa kuleta mpango huu jijini Mwanza, Benki ya Stanbic imethibitisha tena kujitolea kwake kupanua elimu ya fedha, kuhakikisha kuwa familia nyingi zaidi kote Tanzania zinapata ujuzi muhimu wa usimamizi wa fedha.