×

Aziz Ki na Mobetto Waoneshana Mahaba Mazito Mtandaoni, Watumiana Ujumbe

Nyota wa klabu ya Yanga SC na raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki akiwa na mke wake Hamisa Mobetto

Nyota wa klabu ya Yanga SC na raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, baada ya kufunga ndoa hivi karibuni na mwanamitindo, muigizaji, na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Hamisa Mobetto, amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram usiku wa kuamkia leo, Februari 25, 2024.

Katika ujumbe wake, Aziz Ki ameonyesha furaha yake kwa safari yao ya mapenzi, akisema kuwa wanakaribia kutimiza mwaka mmoja tangu walipoanzisha mahusiano yao.

“Siamini zimebaki wiki chache tu tufikie kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu tuanze safari yetu ya mapenzi pamoja. Mwaka huu umekuwa wa kipekee sana nimekuwa mtu bora zaidi kwa sababu yako. Ninashukuru sana kwa safari yetu hii, na natarajia kwa hamu mambo mazuri yajayo.

Asante kwa uvumilivu wako, kwa kuwa mshauri wangu bora, na kwa kusimama nami, hasa nyakati ngumu ambapo ilihisi kama dunia iko dhidi yangu. Asante kwa kunikumbusha kuwa kila changamoto ni ya muda tu, na zaidi ya yote, asante kwa kusema ‘ndiyo’ kuwa mke wangu.

Je serai toujours reconnaissant envers Dieu de t’avoir amenée dans ma vie. Je prie qu’Il continue de nous bénir et de nous garder ensemble, maintenant et pour toujours. (Nitakuwa daima mwenye shukrani kwa Mungu kwa kukuleta katika maisha yangu. Naomba aendelee kutubariki na kutulinda pamoja, sasa na milele).”

Mwisho wa ujumbe wake, Aziz Ki alimwonyesha upendo wa dhati kwa mke wake, akimalizia kwa maneno:

“Nakupenda sana Hamisa, nakupenda sana mke wangu mzuri ❤️✨ @hamisamobetto ✨❤️.”

Muda mfupi baada ya Aziz Ki kuposti ujumbe huo mzito, Hamisa Mobetto alijitokeza kwenye sehemu ya maoni (comments) kumjibu mume wake kwa maneno ya mapenzi.

“Aww, my love, this warms my heart. ❤️ Thank you for being my rock, my best friend, and for choosing me. I’m so grateful for everything we’ve shared, and I pray God keeps blessing and guiding us always. Nakupenda sana, mume wangu wa milele. ❤️✨💍”

Mapenzi yao yanaendelea kuiteka mitandao ya kijamii huku mashabiki wakiwapongeza na kuwatakia kila la heri katika ndoa yao mpya.