×

Tuzo za Trace Afrika 2025 Zakatizwa Zanzibar Baada ya Maji Kujaa, Orodha Washindi Ipo Hapa

Tuzo za Trace za wasanii wa Afrika, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo katika Visiwa vya Zanzibar, Tanzania, zilikumbwa na changamoto kubwa baada ya maji kujaa karibu na jukwaa, hali iliyosababisha kusitishwa kwa hafla hiyo ghafla.

Awali, kulikuwa na dalili za changamoto baada ya upepo mkali na mawimbi kuanza kuvuruga maandalizi, jambo lililosababisha kucheleweshwa kwa kuanza kwa hafla hiyo. Badala ya kuanza saa 2 usiku kama ilivyopangwa, sherehe hizo zilianza rasmi saa 4 usiku, ikiwa ni takriban saa mbili baadaye.

 

Muda mfupi baada ya kuanza, msanii wa Tanzania, Marioo, alifungua tamasha kwa kutumbuiza, kisha wakafuatia wasanii wengine. Hata hivyo, wakati sherehe zikiwa bado katika hatua za mwanzo za kutangaza washindi, ghafla tamasha lilisimamishwa mnamo saa 9:20 usiku, hali iliyoibua maswali mengi miongoni mwa waliokuwepo.

Hakuna maelezo rasmi yaliyotolewa moja kwa moja kutoka jukwaani kuhusu sababu ya usitishaji huo, jambo lililozua minong’ono na malalamiko kwa baadhi ya wageni na mashabiki waliokuwa wamejitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

 

Hata hivyo, kabla ya kukatishwa, baadhi ya washindi walikuwa tayari wametangazwa. Msanii wa Nigeria, Rema, alitangazwa kama Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka, na pia alitwaa tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kupitia albamu yake Heis. Mtayarishaji Bora wa Muziki alitangazwa kuwa P.Priime kutoka Nigeria kupitia kazi yake MMS.

Kwa upande wa wasanii kutoka nchi zinazozungumza Kifaransa, Josey kutoka Ivory Coast alishinda tuzo hiyo, huku Joe Dwet File, mwenye asili ya Haiti na makazi yake Ufaransa, akiibuka mshindi katika kipengele cha Msanii Bora wa Diaspora (wanaoishi nje ya bara la Afrika). Kwa upande wa Brazil, msanii Duquesa alitwaa tuzo hiyo.

Hafla hiyo, ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika Tanzania, iliwaleta pamoja wasanii wengi wakubwa wa Afrika, wakiwemo Diamond Platnumz, Harmonize wa Tanzania, na Bien kutoka Kenya, ambao walitoa burudani ya hali ya juu kabla ya tamasha hilo kusitishwa ghafla.

Mashabiki na wadau wa muziki bado wanatafuta majibu juu ya mustakabali wa tuzo hizo na iwapo zitatangazwa upya au kutakuwa na ratiba nyingine ya kuendelea na hafla hiyo.

Hapa chini ni orodha kamili ya washindi:

Tuzo za Kimataifa

Wimbo wa Mwaka:

Titom & Yuppe – ‘Tshwala Bam’ (Afrika Kusini)
Tyla – ‘Jump’ (Afrika Kusini)
Tyler ICU – ‘Mnike’ (Afrika Kusini)
Tamsir x Team Paiya – ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast)
Asake & Travis Scott – ‘Active’ (Nigeria)
Tems – ‘Love Me Jeje’ (Nigeria)
Burna Boy – ‘Higher’ (Nigeria)
Rema & Shallipopi – ‘Benin Boys’ (Nigeria)
Diamond Platnumz – ‘Komasawa’ (Tanzania)

Albamu ya Mwaka:

Rema – Heis (Nigeria)
Burna Boy – I Told Them (Nigeria)
Asake – Lungu Boy (Nigeria)
Josey – Vibration Universelle (Ivory Coast)
Amaarae – Fountain Baby (Ghana)
King Promise – True To Self (Ghana)
Stonebwoy – 5th Dimension (Ghana)
Toofan – Stamina (Togo)

Ushirikiano Bora:

Tamsir & Team Paiya – ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast)
Titom & Yuppe & Burna Boy – ‘Tshwala Bam’ (Remix) (Afrika Kusini/Nigeria)
Neyna & MC Acondize – ‘Nu Ka Sta Para’ (Cape Verde)
Kocee ft. Patoranking – ‘Credit Alert’ (Cameroon/Nigeria)
Asake & Wizkid – ‘MMS’ (Nigeria)
Rema & Shallipopi – ‘Benin Boys’ (Nigeria)
Odumodublvck & Black Sherif – ‘Woto Woto Seasoning’ (Ghana)

Video Bora ya Muziki:

Meji Alabi – Rema ‘DND’ (Nigeria)
TG Omori – Kizz Daniel & Davido ‘Twe Twe’ (Nigeria)
Director Folex – Zuchu feat Innoss’ B ‘Nani’ (Remix) (Tanzania/DRC)
Nabil Elderkin – Tyla ‘Jump’ (Afrika Kusini)
Kmane – Ayra Starr ‘Commas’ (Nigeria)
Seoute Emmanuel – Toofan ‘C Pas Normal’ (Togo)
Ach’B – Innoss’ B ‘Sete’ (DRC)
Edgar Esteves – Asake & Wizkid ‘MMS’ (Nigeria)

Mcheza Bora:

Makhadzi (Afrika Kusini)
Ikorodu Boys (Nigeria)
Dancegod Lloyd (Ghana)
Incredible Zigi (Ghana)
Kamo Mphela (Afrika Kusini)
Telminho (Angola)
Ordinateur (Ivory Coast)
Issac Kalonji (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)

DJ Bora:

DJ Moh Green – ‘Kelele’ (Algeria)
Tyler ICU – ‘Mnike’ (Afrika Kusini)
Uncle Waffles – ‘Wadibusa’ (Afrika Kusini)
DJ Tunez – ‘Apala Disco Remix’ (Nigeria)
DJ Nelasta – ‘Eros’ (Angola)
DJ Spinall ft. Tyla & Omah Lay – ‘One Call’ (Nigeria)
DJ Neptune ft. Qing Madi – ‘Honest’ (Nigeria)
DJ Maphorisa – ‘Mnike’ (Afrika Kusini)
Kabza De Small – ‘Imithandazo’ (Afrika Kusini)

Msanii Bora wa Hip Hop (inayodhaminiwa na Hot 97):

Didi B (Ivory Coast)
Nasty C (Afrika Kusini)
Odumodublvck (Nigeria)
Suspect 95 (Ivory Coast)
Sarkodie (Ghana)
Young Lunya (Tanzania)
Maglera Doe Boy (Afrika Kusini)

Tuzo za Pan-Afrika

Msanii Bora wa Kimataifa wa Kiafrika:

Diamond Platnumz (Tanzania)
Tyla (Afrika Kusini)
Tyler ICU (Afrika Kusini)
Fally Ipupa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)
Burna Boy (Nigeria)
Asake (Nigeria/USA)
Rema (Nigeria)
Ayra Starr (Nigeria)

Msanii Bora wa Kiume:

Rema (Nigeria)
Dlala Thukzin (Afrika Kusini)
Fally Ipupa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Asake (Nigeria)
Burna Boy (Nigeria)
Wizkid (Nigeria)
Stonebwoy (Ghana)

Msanii Bora wa Kike:

Tyla (Afrika Kusini)
Makhadzi (Afrika Kusini)
Chelsea Dinorath (Angola)
Josey (Ivory Coast)
Ayra Starr (Nigeria)
Tems (Nigeria)
Yemi Alade (Nigeria)

Tuzo za Kanda

Msanii Bora Afrika Mashariki:

Bien (Kenya)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Joshua Baraka (Uganda)
Harmonize (Tanzania)
Rophnan (Ethiopia)
Marioo (Tanzania)
Zuchu (Tanzania)
Nandy (Tanzania)

Tuzo ya Msanii Bora wa Afrika Magharibi (Inglophone):

Ayra Starr (Nigeria)
Seyi Vibez (Nigeria)
Adekunle Gold (Nigeria)
Tems (Nigeria)
Chike (Nigeria)
Simi (Nigeria)
KiDi (Ghana)

Tuzo ya Msanii Bora wa Afrika Kusini:

Tyler ICU (Afrika Kusini)
Titom & Yuppe (Afrika Kusini)
De Mthuda (Afrika Kusini)
Inkabi Zezwe (Afrika Kusini)
Dlala Thukzin (Afrika Kusini)
Tyla (Afrika Kusini)
Uncle Waffles (Afrika Kusini)

Tuzo za Kimataifa na Diaspora

Msanii Bora wa Ulaya:

Joe Dwet File (Ufaransa/Haiti)
Central Cee (Uingereza)
Kalash (Ufaransa/Matiniki)
Darkoo (Uingereza)
Jungeli (Ufaransa)
Franglish (Ufaransa)
Aya Nakamura (Ufaransa/Mali)

Msanii Bora wa Brazil:

Duquesa (Brazil)
Racionais MC’s (Brazil)
MC IG (Brazil)
Péricles (Brazil)
Tasha & Tracie (Brazil)
Ludmilla (Brazil)

Msanii Bora wa Karibiani:

Lea Churro (Kisiwa cha Reunion)
Venssy (Guiana ya Kifaransa)
Mathieu White (Guadeloupe)
Meryl (Matiniki)
Nesly (Guiana ya Kifaransa)
Shenseea (Jamaica)
Kenny Haiti (Haiti)

Msanii Bora wa Bahari ya Hindi:

Barth (Reunion)
Goulam (Comoros)
PLL (Reunion)
Kalipsxau (Reunion)
Léa Churros (Reunion)
Jamily Jeanne (Mauritius)

Tuzo za Maisha

Tuzo ya Mafanikio ya Maisha:

D’Banj