×

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Alivyowasili nchini Namibia ambapo kumwakilisha Rais Samia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango Februari 27, 2025 amewasili Jijini Windhoek nchini Namibia ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma.

Utoaji wa heshima za mwisho na Ibada ya kumuaga Kitaifa hayati Dkt. Nujoma itafanyika katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru uliopo Jijini Windhoek tarehe 28 Februari 2025 na Mazishi yatafanyika katika eneo la Makaburi ya Mashujaa yaliyopo katika Jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 01 Machi 2025.