×

Viongozi Ulaya wamuunga mkono Zelensky kufuatia mzozo wake na Trump Ikulu

Zelensky akiondoka Ikulu ya Marekani, bila kuagwa na mwenyeji wake Trump kama ilivyo kwa viongozi wakuu wanapotembeleana

Muda mfupi baada ya mkutano kati ya Donald Trump na Volodymyr Zelensky kuvunjika kwa kurushiana maneno makali, viongozi wa Ulaya wazungumza.

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Waziri Mkuu wa Polandia na rais wa zamani wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, alimuandikia Zelensky na kusema, “Marafiki wapendwa wa Ukraine, hamko peke yenu.”

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Akiulizwa kuhusu mvutano huo alipokuwa Ureno, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, aliviaambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa Urusi ndiyo anayeshambulia na kwamba watu wa Ukraine ndio wanaoshambuliwa.

Ameongeza kuwa nchi za Ulaya na washirika wengine walikuwa sahihi kwa kuisaidia Ukraine miaka mitatu iliyopita, kuwapatia vikwazo Urusi na kuendelea kufanya hivyo.

Aidha, ameongeza kuwa ni muhimu “kuheshimu” wale ambao wamekuwa wakipigania tangu mwanzo kwa ajili ya heshima, haki na usalama wa Ulaya.

https://globalpublishers.co.tz/mkutano-kati-ya-trump-na-zelensky-kuhusu-makubaliano-ya-madini-waisha-ghafla/