×

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Samia katika maombi maalum ya kuliombea Taifa Viwanja wa Leaders

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Februari 28, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maombi maalum ya kuliombea Taifa yaliyondaliwa na Umoja wa Viongozi wa Makanisa, kwenye Viwanja wa Leaders, jijini Dar es Salaam.

“Ninatoa rai kwa viongozi wa dini na Watanzania wote msichoke kuiunga mkono serikali yenu, ili sote tuendelee kuishi pamoja kwa amani, upendo na mshikamano. Serikali inatambua wajibu mkubwa wa kiroho mlionao ambao unaleta matokeo chanya katika maisha yetu ya kila siku, endeleeni kujitoa kwa ajili ya Taifa letu, viongozi na wananchi wake, hatuna mashaka na imani yenu na mapenzi yenu kwa serikali” amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa